Shambulio la Israel kaskazini mwa Gaza ladokeza mpango wa jenerali mstaafu wa "kujisalimisha au kufa njaa" kwa ajili ya vita.
umamosi asubuhi, ujumbe ulitumwa kwenye mitandao ya kijamii na msemaji wa Kiarabu wa jeshi la Israel akiwaonya watu wanaoishi katika eneo la 'D5' kaskazini mwa Gaza kuhamia kusini.
Majengo ya D5 ni ya mraba yaliyoko kwenye ramani za Gaza na Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF). Majengo haya ni kizuizi ambacho kimegawanywa katika maeneo kadhaa madogo.
Ujumbe huo ambao ni wa hivi punde zaidi katika mfululizo, ulisema: "IDF inafanya kazi kwa nguvu kubwa dhidi ya mashirika ya kigaidi na itaendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu. Eneo lililotengwa, ikiwa ni pamoja na makazi yaliyoko huko, linachukuliwa kuwa eneo hatari la mapigano. Wakazi wa eneo hilo zima wahamishwe mara moja kupitia Barabara ya Salah al-Din hadi eneo la kibinadamu."
Eneo la kibinadamu lililoteuliwa na Israel katika ujumbe huo ni al-Mawasi, ambalo hapo awali lilikuwa eneo la kilimo kwenye pwani karibu na Rafah. Iimejaa watu wengi na halina usalama zaidi kuliko sehemu nyingine nyingi za Gaza.
BBC Verify imefuatilia na kuthibitisha angalau mashambulizi 18 ya anga katika eneo hilo
TANGAZA BIASHARA NASI KATIKA BLOG
YETU YA MAGENHIRO BLOG IYO JALI KILA
MTU KARIBU SASA ILI UHUDUMIWE HARAKA
TUPIGIE AU WHATSAPP+255768163863
Chapisha Maoni