wanini unapaswa kubadilisha mashuka ya kitandani mara kwa mara?

dfcv

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Author, Jasmin Fox-Skelly
  • Nafasi, BBC

Juu ya mashuka yetu na mito ni mahali tunapotumia theluthi moja ya maisha yetu ya kila siku. Baada ya siku ndefu, hakuna kitu kizuri kama kujitupa juu ya kitanda, kuegemeza kichwa chako kwenye mto laini na kujikunyata ndani ya shuka laini.

Lakini jambo la kuogofya kuhusu kitanda chako ni kwamba kuna mamilioni ya bakteria, fangasi, wadudu na virusi. Kila mmoja wao anadhani kitanda chako ni peponi kwake; mahali penye joto ambapo wanaweza kukua, pamejaa jasho, mate, chembechembe za ngozi zilizokufa na ndio chakula kwa ajili yao.

Mfano, vijidudu vidogo sana vinavyoishi kwenye vumbi. Tunamwaga seli za ngozi milioni 500 kwa siku, vijidudu hivyo hula seli hizo. Kwa bahati mbaya, vidudu hivyo na mabaki yake (kinyesi) vinaweza kusababisha mzio, pumu na ukurutu.

Mashuka ya kitanda ni kimbilio la bakteria pia. Mwaka 2013, watafiti katika Taasisi ya Pasteur de Lille huko Ufaransa walichunguza mashuka ya kitanda cha hospitali na kugundua yamejaa bakteria wa Staphylococcus, ambao hupatikana zaidi kwenye ngozi ya binadamu.

Ingawa spishi nyingi za staphylococcus hazina madhara, lakini baadhi, kama vile S. aureus, wanaweza kusababisha maambukizi ya ngozi, chunusi na hata nimonia kwa wagonjwa walio na kinga dhaifu.

"Watu hubeba bakteria wengi katika ngozi zao," anasema Manal Mohammed, mwanabiolojia wa Chuo Kikuu cha Westminster nchini Uingereza.

"Ingawa bakteria hawa kwa kawaida hawana madhara, ila wanaweza kusababisha ugonjwa mbaya ikiwa wataingia mwilini kupitia majeraha ya wazi, ambayo ni ya kawaida katika hospitali," anasema Manal

KARIBUNI NYOTE KATIKA BLOG HII PENDWA TWAPATIKANA WHATSAP +255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top