Jinsi washirika walivyogeuka maadui katika taifa la Afrika lenye utajiri wa Almasi
- Author, Damian Zane in London & Innocent Selatlhwa in Gabarone
- Nafasi, For BBC News
Sauti ya upole ya Ian Khama haifichi tena ghadhabu aliyonayo.
Katika mahojiano kadhaa tangu 2019, rais wa zamani wa Botswana hakusita kuelezea kutoridhishwa kwake na mrithi wake Mokgweetsi Masisi.
Masisi alikuwa "ameleweshwa na madaraka", Khama aliambia kipindi cha BBC cha Focus on Africa miaka mitano iliyopita.
Tangu wakati huo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71 amekibilia uhamishoni, kudai kwamba kuna njama ya kumtilia sumu au kumkamatwa na kumshtaki nchini Botswana kwa makosa kadhaa ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utakatishaji fedha na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Alipuuzilia mbali mashtaka hayo na kuyataja kuwa "hujuma", mwezi uliopita alirejea nyumbani na kufika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza.
Mvutano kati ya Khama na Masisi huenda ukatia doa uchaguzi mkuu unaokaribia wa nchi hiyo yenye utajiri wa almasi – majuma matatu pekee – huku rais huyo wa zamani akifanyia kampeni chama cha upinzani.
Kwa muda mfupi zaidi, kufika mahakamani Jumanne, Khama alikuwa akitabasamu.
Mamlaka sasa inasadikiwa kuzingatia ikiwa kesi hiyo ingeendelea.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba shughuli zitasisitishwa kwani washtakiwa wenzake Khama hawakabiliwi tena na mashtaka. Lakini mahakama haitakutana tena hadi mwezi mmoja baada ya uchaguzi.
Kwa mtu wa nje, Botswana ni mojawapo ya nchi zilizo na demokrasia imara zaidi ya barani yenye taasisi zenye nguvu, mzozo huu kati ya rais wa sasa na rais wa zamani unaweza kuonekana wa kushangaza.
Chama cha Botswana Democratic Party (BDP) kimetawala tangu uhuru kutoka kwa Uingereza mwaka 1966.
Katika mfumo wa eneo bunge, imetawala bunge kwa miongo mitano iliyopita ingawa sehemu yake ya kura katika chaguzi za hivi majuzi imekuwa karibu 50%.
Rais wa kwanza wa nchi hiyo, na babake Khama, Sir Seretse Khama, alitokana na familia ya kifalme na alisaidia kuimarisha sifa ya Botswana ya serikali yenye utaratibu katika miaka 14 aliyokuwa madarakani hadi kifo chake mwaka 1980.
Ndoa yake ya 1948 na Muingereza, Ruth Williams, ilikuwa na utata hadi ikachangia uhamisho wake nchini Uingereza.
Ian Khama, mtoto wa pili wa wanandoa hao, alifananisha wakati wake wa hivi majuzi nchini Afrika Kusini na ule wa baba yake akiwa mbali na Botswana.
Baada ya kuwa jeshini, aliendelea kuwa rais mnamo 2008, akihudumu kwa miaka 10.
Licha ya rufaa ya iliyowasilishwa kupinga ugombea wa Khama chama chake cha BDP kilipata chini ya 50% ya kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa 2014.
Wasiwasi kuhusu rushwa, haki za binadamu na hali ya uchumi - viwango vya juu vya ukosefu wa ajira - yote yalidhoofisha umaarufu wa Khama.
Hifadhi kubwa ya almasi nchini imeonekana kuwa ya faida na kiungo muhimu kwa ukuaji wa uchumi, lakini hakuna nafasi za ajira za kutosha zilizobuniwa kwa idadi kuwa ya vijana na utajiri huo haukusambazwa kote.
Mnamo 2018, Khama alimkabidhi makamu wake mwaminifu, Masisi hatamu za uongozi, labda akitumai kuwa anaweza kuwa na ushawishi, lakini mambo yalienda mrama.
Makubaliano kati ya washirika hao ni kwamba Masisi angemteua kakake Khama, Tshekedi, kama makamu wa rais, jambo ambalo alikataa kufanya.
Khama alianza kulalamika kuwa maafisa wake wa usalama wanapunguzwa na kwamba demokrasia ndani ya chama cha BDP inaminywa.
Masisi pia alibadilisha baadhi ya sera muhimu kama vile kupiga marufuku uwindaji wa tembo na kusitisha uhusiano wa karibu na China.
Mwaka mmoja baada ya kujiuzulu kama rais, Khama alijiunga na chama kipya cha upinzani cha Botswana Patriotic Front (BPF) akiambia BBC wakati huo kwamba "demokrasia ambayo tumekuwa tukijivunia katika nchi hii sasa inadora".
Baadaye akaenda uhamishoni mwisho mwa mwaka 2021 kwa madai ya kutishiwa maisha.
Masisi amekanusha madai hayo mwanzoni mwa mwaka huu akielezea madai ya kama "ya kushtua".
"Ukiangalia historia ya mauaji nchini Botswana na mbinu zinazotumika, kumtilia mtu sumu si mojawapo ya zile zinazotumiwa, lakini hivi karibuni yeye [Khama] anaonekana kuwa mtaalamu," Masisi aliiambia France 24, akiongeza kwamba rais huyo wa zamani hakuwa na chochote cha kuogopa.
Masisi pia alisema kuwa hoja ambazo Khama amekuwa akizitumia dhidi ya serikali na uongozi wake umekuwa "ukutofautiana".
Hakuna matumaiani ya maridhiano kati ya washirika wa zamani, na Khama anatarajia kumaliza miaka 58 madarakani ya BDP - chama ambacho baba yake alisaidia kupatikana.
Kuna fursa za kuchukua kura kutoka kwa serikali kwani shida za ukosefu wa ajira na tuhuma za ufisadi pia zimetawala utawala wa sasa.
Zaidi ya hayo, rais huyo wa zamani bado anaheshimika sana nchini, haswa miongoni mwa wapiga kura wazee na katika eneo la nyumbani kwake karibu na Serowe, ambapo yeye ndiye chifu mkuu na ambapo BPF ilizindua ilani yake mwishoni mwa wiki.
Lakini Masisi na BDP wanasalia katika msimamo mkali, haswa kwani upinzani umegawanyika.
Chapisha Maoni