Sean 'Diddy' Combs atuhumiwa kumnyanyasa kingono mvulana katika kesi mpya

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Sean "Diddy" Combs anakabiliwa na madai mapya ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia na mateso ya kingono baada ya msururu wa kesi mpya kuwasilishwa Jumatatu.

Takriban kesi sita ziliwasilishwa katika mahakama ya shirikisho ya New York na wanawake wawili na wanaume wanne. Kesi hizo zinajumuisha madai ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2021.

Walalamikaji hao ambao hawakutajwa wanadai kuwa baadhi ya unyanyasaji huo ulitokea kwenye sherehe za Bw Combs, ambazo zilihudhuriwa na watu mashuhuri na wasanii wa muziki.

Mawakili wa Bw Combs walikanusha madai hayo, wakisema katika taarifa kwa BBC kwamba "hajawahi kumnyanyasa mtu yeyote kingono - mtu mzima au mdogo, mwanamume au mwanamke".

Mmoja wa wanaomshitaki alisema alikuwa na umri wa miaka 16 alipohudhuria moja ya karamu katika eneo la Hamptons mnamo 1998.

Katika kesi hiyo, anaelezea kuwa alifurahi kupata mwaliko wa hafla ya Bw Combs, ambayo ilikuja kuwa hafla kuu ya kila mwaka ya watu mashuhuri.

Alisema kuwa aliwaona watu mashuhuri na wasanii wengi wa muziki alipokuwa akitembea tembea, na akakutana na Bw Combs alipokuwa njiani kuelekea bafuni. Alisema alianza kuzungumza na Bw Combs kuhusu kuingia kwenye tasnia ya muziki ambapo walipoenda mahali pa faragha zaidi. Anadai kuwa wakati wa mazungumzo yao, Bw Combs alimuamuru ghafla avue nguo.

Kesi hiyo inajumuisha picha ya wawili hao wakiwa pamoja kwenye karamu huku uso wa kijana huyo ukionekana kufichwa.

Kulingana na shtaka hilo, Bw Combs alisema ni "utaratibu wa kupitia" na ni "njia ya kuwa nyota." Rapper huyo alimwambia kijana huyo kuwa anaweza kumfanya mtu yeyote kuwa nyota na akamwambia kijana ana "mwonekano" unaofaa [ kwa hilo], kesi hiyo inasema.

Kesi nyingine iliyowasilishwa Jumatatu ni pamoja na kuhusu madai ya mwanamke ambaye anadai Bw Combs alimbaka katika chumba cha hoteli mwaka wa 2004 alipokuwa mwanafunzi wa chuo mwenye umri wa miaka 19. De

KARIBU SANA KATIKA BLOG YA MÄGËNHÏRÖ BLOG TUNAKUJARI TUNAKUTHAMINI WHATSAPP +255 768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top