Urusi imeitaka Marekani kupunguza maafisa wake katika ubaloziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUrusi imeitaka Marekani kupunguza maafisa wake katika ubalozi
Urusi imetangaza kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo vipya ilivyowekewa na bunge la Congress la Marekani.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Urusi ilitangaza hatua hiyo, baada ya bunge la Congress la Marekani kupitisha vikwazo vipya dhidi yake.
Urusi imetangaza kuwa Marekani italazimika kupunguza idadi ya maafisa wa kibalozi walio nchini mwake hadi 455, idadi ambayo kwa sasa Urusi inaruhusiwa kuwa nao Marekani.
Wizara hiyo ilisema kuwa kuanzia Agosti, Ubalozi wa Marekani hautaruhusiwa kutumia maghala yake jijini Moscow au katika boma la ubalozi wake sehemu za mashambani nchini Urusi.
Rais Vladimir Putin alisema jana kuwa ni vigumu kwa Urusi kuendelea kuwa na uvumilivu dhidi ya vikwazo inavyowekewa na Marekani.Miezi saba iliyopita Rais Obama aliwatimua maafisa 35 wa ubalozi wa Urusi na kutaifisha nyumba mbili za Urusi kwa kulaumu taifa hilo kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana.
Russia imeitaka Marekani kupunguza idadi ya wafanyikazi wake katika ubalozi hadi 455 mbali na kuweka marufuku kuhusu utumizi wa majumba fulani.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi pia amesema kuwa atayazuia majumba yanayotumiwa na maafisa hao wakati wa likizo mbali na ghala moja linalotumika na wanadiplomasia hao wa Marekani.
Vikwazo hivyo vinafuatia hatua ya Urusi kulinyakua eneo la Crimea mbali na kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Hatua hiyo ya Urusi inajiri miezi kadhaa baada ya utawala wa rais Obama kuagiza kuzuiliwa kwa nyumba mbili za kidiplomasia na kufurushwa kwa wanadiplomasia 35 wa Urusi kujibu hatua ya Urusi kudukua kampeni za chama cha Democratic kilichokuwa kikiongozwa na mgombea wake Hillary Clinton.

    Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

    Chapisha Maoni

     
    Top