Image result for yangaMABINGWA wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Yanga wamesema kutokuwafahamu vizuri wapinzani wao mabingwa wa Kenya, Tusker kunaweza kusababisha mchezo wao kuwa mgumu.
Yanga imeanza mazoezi jana kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania Kombe la SportPesa utakaochezwa kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Tayari Tusker ipo jijini tangu juzi ikiendelea na mazoezi yake kuelekea kwenye mchezo huo wa mashindano hayo yatakayoshirikisha jumla ya timu nane, nne za Tanzania na nne za Kenya.
Akizungumza na gazeti hili jana Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi alisema hawakubahatika kuwafuatilia sana wapinzani wao hao, akisema pengine siku mbili hizi yaani jana na leo wanaweza kutafuta taarifa zao kujua hutumia mbinu gani.
“Hatujajua aina ya soka lao, lakini kabla ya kukutana nadhani tutakuwa tumejua, kikubwa kwetu ni kujipanga,”alisema. Pamoja na hilo, alisema kukosekana kwa baadhi ya wachezaji waliokwenda kutumikia timu zao za taifa kunaweza kuathiri kikosi chake.
Baadhi ya wachezaji hao ni Haruna Niyonzima (Rwanda), Thaban Kamusoko (Zimbabwe), Beno Kakolanya, Simon Msuva na Hassan Kessy (Taifa Stars). Mwingine ambaye alikwenda mapumziko ni Amis Tambwe (Burundi).
Mwambusi alisema wachezaji waliopo wako tayari kwa mchezo huo na kwamba watawatumia vijana na wakubwa katika kulipigania kombe hilo na fedha sh. Sh milioni 66. Aliomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono katika mechi hiyo itakayochezwa saa 10.00 jioni.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top