NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega, mkoani Tabora amempongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua kulinda rasilimali za umma.
Kigwangalla amesema kuwa duniani kuna nchi moja tu ambayo Rais wake alikataa kuibiwa na alifanikiwa kupatanisha upya (re-negotiate) mikataba yote ya raslimali za Taifa zilizokuwa zinavunwa na makampuni makubwa ya kimataifa.
Aliitaja nchi ya Bolivia huko Amerika ya Kusini kuwa Rais wake Juan Evo Morales Ayma ambaye ni maarufu kama Evo Morales, amekuwa maarufu sana kwa watu wake na sababu kubwa ikiwa uzalendo na upendo wake wa dhati kwa watu wa chini, ambao leo amewakomboa kwa kutumia Raslimali za nchi zilizokuwa zinaibwa 'kihalalali' kwa njia ya mikataba kabisa!
"Namfananisha Rais wetu John Magufuli na Rais wa Bolivia Evo Morales kwa hatua anazozichukua dhidi ya ulinzi wa rasilimali za taifa," alisema Dk Kigwangalla. "Tumeweza kupata ukweli wa kilichokuwa kinaendelea sababu, Rais ameunda Kamati yenye watu mbalimbali, hapo hakukuwa na kununuliwa. Kila mtu anamuogopa mwenzake, alisema Kigwangalla.
Alishauri utaratibu uliotumika katika kamati hiyo pia ukatumika wakati wanawahoji watu wote walioguswa kwenye ripoti za Kamati na timu ya mashushushu iwe ya mchanganyiko - kuwa na CID, Usalama wa Taifa, Jeshi na PCCB.
Aidha alisema kuwa anayehojiwa awe anatokea mbele ya panel ya wachunguzi. Siyo mchunguzi mmoja kwani kufanya hivyo kutaepusha upendeleo na kuharibu taarifa.
"Huu ni wakati wa watanzania wote kwa pamoja kusimama na Rais wetu bila kujali itikadi za vyama vyetu, maana sote tunaungana kwenye mahitaji ya maendeleo na ustawi wa maisha ya watanzania wote. Vita hii si ndogo na si yake peke yake, ni yetu sote,"alisema Dk Kigwangalla.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Chapisha Maoni