MIRADI sita yenye jumla ya thamani ya Sh bilioni 7.6 ukiwamo mradi wa ujenzi wa mtambo wa uchakataji wa maji taka wa kiwanda cha 21 century umezinduliwa mwishoni mwa wiki katika mbio za Mwenge wa Uhuru.
Mwenge huo ambao umeingia mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki kwa sasa upo Manispaa ya Morogoro. Akitoa taarifa ya mradi huo uchakataji maji taka, Ofisa utumishi wa kiwanda hicho, Stephen Mrambiti alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuwezesha maji hayo kutumika tena kwa matumizi mengine kiwandani. Ujenzi wa mtambo huo ulianza Machi mwaka jana na kwamba unafanywa kwa awamu.
Mradi huo unaotarajiwa hadi utakapokamilika mwaka huu utakuwa umegharimu kiasi cha dola za marekani 272,700. Mwenge wa uhuru pia umezindua mradi wa mafunzo ya ushonaji na ajira kwa vijana katika kiwanda cha nguo za michezo cha Mazava ambao umegharimu kiasi cha Sh 5,555,892,000. Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja ajira, Mashauri Mchele alisema kuwa lengo la mradi huo ni kutoa mafunzo ya ushonaji wa nguo za michezo kwa vijana, kutoa ajira ya ushonaji wa nguo za michezo pamoja na kuwawezesha vijana kupata ujuzi wa ushonaji nguo na baadae kuweza kujiajiri wenyewe.
Aidha alisema kuwa kiwanda kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kilianzisha mpango wa kutoa mafunzo ya ushonaji wa nguo kwa vijana wa Kitanzania ili kwa kupitia mafunzo hayo vijana waweze kupata ujuzi wa kuajiriwa na kujiajiri. Alisema kuwa jumla ya vijana 366 wamepata mafunzo hayo kati yao vijana 180 wameajiriwa kiwandani hapo na kwamba waliosalia wamejiajiri wenyewe. Naye Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Amoor Amed Amoor aliwataka vijana hao kujiepusha na ukimwi, rushwa na kufanya kazi kwa bidii.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Chapisha Maoni