KOCHA wa timu ya Taifa Stars, Salum Mayanga awashangaa wanaobeza kuitwa kwa mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza soka la Kimataifa kwenye klabu ya AFC Eskilstuna ya nchini Sweden.
Mayanga alisema hakufanya uamuzi huo kwa kurupuka kwani alishafanya mazungumzo naye ili kujua mwenendo wa afya yake nchini Sweden. “Nilifanya mazungumzo na Ulimwengu siku tatu kabla ya kumwita kwenye kikosi cha timu ya Taifa lakini pia nilipata muda wa kuzungumza na viongozi wa klabu yake,” alisema Mayanga.
“Niliridhika na hali yake baada ya kuelezwa ameanza mazoezi siku 10 nyuma na uchunguzi wa goti lake wanakasema yuko vizuri kwa ajili ya kucheza,” aliongeza. Ulimwengu hakuwepo kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa muda mrefu tangu apate jeraha la goti na kwenye klabu yake amekuwa nje kwa sababu ya tatizo hilo.
Baadhi ya wadau wa soka walishangaa uamuzi wa Mayanga kumjumuisha kikosini Ulimwengu ambaye amekuwa benchi kwa muda mrefu kutokana na jeraha la goti.






Chapisha Maoni