SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka (Fifa) limezipongeza timu nne zilizofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zinazofanyika Gabon.
Timu za Ghana, Mali, Guinea na Niger zimefuzu kucheza hatua hiyo na moja kwa moja zimekata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa umri huo zitakazofanyika India kuanzia Oktoba 6-28 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Fifa, shirikisho hilo limezipongeza timu hizo na kuzitakia kila la heri katika fainali hizo pamoja na zile za Fifa za Kombe la Dunia zitakazofanyika India. Ushindi katika mechi zao za mwisho za makundi Jumapili, ziliihakikishia Mali na Niger kufuzu kucheza Kombe la Dunia baada ya kufanikiwa kutinga nusu fainali.
Timu mbili za juu kutoka Kundi B zitaungana na zile za Kundi A za Ghana na Guinea, ambazo pia zitakwenda India. Mabingwa watetezi Mali waliongoza katika Kundi B baada ya kuifunga Angola mabao 6-1 katika mchezo uliofanyika Libreville.
Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo kufuzu kwa mara ya tano kucheza fainali za Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo katika miaka ya 1997, 1999, 2001, na 2015. Kwa kujiunga na Ghana, Guinea, na Mali kukata tiketi ya kwenda India katika fainali zitakazofanyika Oktoba, Niger imeweka historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali hizo za Fifa baada ya kuifunga kwa tabu Tanzania 1-0 katika mchezo uliofanyika Port Gentil na kumaliza ya pili katika Kundi B, ikiwa juu ya Serengeti Boys kwa tofauti ya mabao.
KWAHABARI MATANGAZO ,NYIMBO,WASILIANA NASI;0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top