MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17, Serengeti Boys, Yohana Mkomola hajakata tamaa baada ya kuondolewa katika fainali za Afrika na Niger.
Akizungumza kwa njia ya mtandao, Mkomola alisema wameondolewa katika mashindano ya U-17 Afrika lakini wamejifunza mengi na hawajakata tama kwani kuna mashindano mengine ya umri tofauti watakayoshiriki.
“Mshindi ni yule mwenye ndoto na asiyeweza kukata tamaa na sisi hatujakata tamaa kwani tunatarajia kushiriki mashindano mengine ya U-20 na U-23 tutafanya vizuri,” alisema Mkomola.
Pia Mkomola alisema kufungwa na Niger kuliwafanya wasijikie vibaya kwani wao walihitaji pointi moja lakini wakapoteza na kujikuta wakitupwa nje na kushindwa kuandika historia.
Serengeti Boys ilihitaji sare tu kujihakikishia kufuzu nusu fainali na pia kufuzu Kombe la Dunia baada ya sare ya 0-0 na mabingwa watetezi, Mali na ushindi wa 2-1 dhidi ya Angola lakini wakajikuta wanapoteza kwa kipigo cha 1-0. Hatua ya makundi ya mashindano hayo ilianza wiki moja iliyopita, ambapo Ghana, Guinea, Cameroon na wenyeji Gabon zilishiriki katika Kundi A wakati Tanzania, Mali, Angola na Niger zilicheza katika Kundi B.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA NYIMBO,NK,TUPIGIE;0623372368






Chapisha Maoni