PyongyangHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani kwa sasa huwaonya tu raia wake dhidi ya kuzuru Korea Kaskazini
Marekani inapanga kupiga marufuku raia wake wasisafiri kwenda Korea Kaskazini, kwa mujibu wa mashirika mawili ya kupanga safari ambayo yanafanya kazi humo.
Mashirika hayo ya Koryo Tours na Young Pioneer Tours yamesema marufuku hiyo itatangazwa tarehe 27 Julai na itaanza kutekelezwa siku 30 baadaye.
Seriakli ya Marekani bado haijathibitisha taarifa hizo.
Young Pioneer Tours ndio waliofanikisha mwanafunzi Mmarekani Otto Warmbier kuzuru Korea Kaskazini.Alikamatwa baadaye muda mfupi kabla yake kuondoka nchini humo na akahukumiwa kufungwa jela miaka 15.
Hata hivyo, alirejeshwa Marekani mwezi Juni akiwa amepoteza fahamu na akafariki dunia wiki moja baadaye.
Kampuni hiyo, yenye makao yake China, imesema haitasaidia Wamarekani wengine kuingia Korea Kaskazini.
Ilitoa taarifa Ijumaa na kusema: "Tumefahamishwa sasa hivi kwamba serikali ya Marekani haitawaruhusu tena raia wa Marekani kusafiri DPRK (Korea Kaskazini).
"Inatarajiwa kwamba marufuku hiyo itaanza kutekelezwa katika kipindi cha siku 30 kuanzia Julai 27. Baada ya kipindi hicho cha siku 30 raia yeyote wa Marekani ambaye atasafiri Korea Kaskazini atafutiwa pasipoti yake na serikali ya taifa lake."
Rowan Beard, wa Young Pioneer Tours, ameambia BBC kwamba kampuni hiyo imefahamishwa hayo na ubalozi wa Sweden, ambao hushughulikia masuala ya Marekani nchini Korea Kaskazini.Ubalozi huo unajaribu kubaini idadi ya watalii kutoka Marekani ambao bado hawajaondoka Korea Kaskazini.
Bw Beard amesema ubalozi huo unawahimiza raia wa Marekani kuondoka nchini humo mara moja.
Amesema nafuu hiyo ya siku 30 "itawapa fursa (Wamarekani) wowote ambao kwa sasa wamo nchini humo kama watalii ama wakifanya kazi za kibinadamu."
Simon Cockerill, wa Koryo Tours, ameambia BBC kwamba amepashwa habari na ubalozi wa Sweden.
Amesema shirika hilo bado litaendelea kupanga safari na kupeleka Wamarekani Korea Kaskazini hadi marufuku hiyo ianze kutekelezwa.
Bw Cockerill amesema: "Ni habari za kusikitisha sana kwa sekta hii na pia kwa raia wa Korea Kaskazini ambao wanataka kuwafahamu zaidi Wamarekani.
Otto Frederick Warmbier on 29 February 2016Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionOtto Warmbier alionekana kwenye kikao cha wanahabari 2016 akikiri kuiba bango la propaganda
Otto Warmbier, 22, alikuwa mwanafunzi wa somo la uchumi ambaye alikamatwa 2 Januari, 2016 na akakiri kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwenye hoteli.
Alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu.
Juni, Korea Kaskazini ilisema alikuwa amepoteza fahamu kwa mwaka mmoja baada ya kuugua ugonjwa kwa jina botulism.
Alirejeshwa Marekani 13 Jun1 lakini akafariki wiki moja baadaye bila kupata fahamu tena.
Raia wengine watatu wa Marekani bado wanazuiliwa Korea Kaskazini.
Kim Dong-chul, 62, mmishenari wa Marekani mwenye asili ya Korea, Profesa Mmarekani mwenye asili ya Korea Kim Sang-duk (auTony Kim); naKim Hak-song, aliyekuwa akifanya akzi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST).Marekani imekuwa ikiituhumu Korea Kaskazini kwa kuwazuilia raia wake na kuwatumia kama chambo wakati wa mashauriano kuhusu mpango wa silaha za nyuklia wa Korea Kaskazini.
Wasiwasi na uhasama ulizidi mwezi jana baada ya Korea Kaskazini kutangaza kufanyia majaribio kombora lake la kwanza lenye uwezo wa kutoka bara moja hadi nyingine, hatua iliyokiuka tena marufuku ya Umoja wa Mataifa.
Marekani na Korea Kusini zilijibu kwa kufanya mazoezi ya makombora na pia zikatoa onyo kali kwa Korea Kaskazini.

KWA MATANGAZO YA BIA SHARA NK>>PIGA WHATSAPP, FB0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top