Kombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai shirikisho la soka barani Afrika limethibitisha
Image captionKombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai shirikisho la soka barani Afrika limethibitisha
Kombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai shirikisho la soka barani Afrika limethibitisha.
Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.
Kinyang'anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon kitashirikisha timu 24 badala ya 16.
Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.
Michuano hiyo imekuwa ikishirikisha timu 16 tangu 1996.
Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.
Mashindano hayo yataendelea kila baada ya miaka miwili barani Afrika.
Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.
Tangazo hilo linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais wa Caf Ahmad kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.

KWA MATANGAZO YA BIA SHARA NK>>PIGA WHATSAPP, FB0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top