Mlinzi muIsrael amempiga risasi na kumuua mshambuliaji raia wa Jordan ambaye alimvamia karibu na ubalozi wa Israel nchini Jordan.
Mtu mwingine raia wa Jordan naye aliuwawa wakati wa ufyatuaji risasi kwa mujibu wa Israel. Mlinzi huyo aliripotiwa kujeruhiwa.
Mshambuliaji alikuwa ni seremala aliyekuwa akifanya kazi katika jengo uliko ubalozi wa Israel.
Hiki ni moja ya visa vibaya zaidi kati ya nchi hizo tangu zisaini mkataba wa mani mwaka 1994.Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho.
Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman.
Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.
GETTY IMAGES
Chapisha Maoni