Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionImage result for china eastern airlinesNdege hiyo ilitua salama
Ndege moja ya shirika la China Eastern Airlines ililazimika kurudi mjini Sydney Australia baada ya kupatwa na hitilafu wa mitambo ambayo ilisababisha shimo sehemu ya injini ya ndege hiyo.
Ndege ya MU736 ilikuwa safarini kutoka Sydney ikilekea Shanghai China lakini rubani akaripoti kuhusu matatizo kwenyr injini katibu saa moja baada ya ndege kuanza safari.,
Abiria waliambia vyombo vya habari kuwa walihisi harufu na kitu kinachochomeka ndani ya ndege.
Ndege hiyo aina ya Airbus A330 ilitua salama na hakukuwa na ripti zozote za majeruhi.Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha shimo kubwa upande wa injini.
Abiria kadha walisema kuwa walisikia sauti kubwa ikitokea injini ya upande wa kushoto muda mfupi baada ya ndege kupaa.
Abiria mmoja aliambia shirika la Seven News Network, "ghafla tukaskia sauti hii...kisha tukahisi haribu ya kuchomeka."
Still from Reuters TV footage of China Eastern plane landing at Sydney on 11 June 2017Haki miliki ya pichaREUTERS TV
Image captionChina Eastern Airlines lililisema kuwa abiria watapewa ndege nyingine
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //0623372368=0768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top