Mwanamke mmoja alikatiza mkutano wa umma uliokuwa umehudhuriwa na Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mji mkuu wa Dar es Salaam, kumuomba achukue hatua dhidi ya watu ambao amewalaumu kwa kupanga njama ya kumnyanganya mali yake.
Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina Shosi, alizua kizaa zaa wakati wa siku ya sheria ambayo ni warsha ya kila mwaka, inayoandaliwa na mahakama kutoa mafunzo ya kisheria na misaada ya sheria.
Kwenye video iliyosambazwa katika mitandao, mama huyo alibeba bango lenye maandishi lililosababisha Rais Magufuli kuwaamrisha polisi kumruhusu aende karibu na eneo alikuwa ameketi.
Bi Shosi kisha akaanza kuelezea jinsi mifumo ya mahakama imehujumu kesi yake kwa kutoa amri zinazokinzana na kuwa amapokea vitisho kwa maisha yake.
Gazeti la serikali la Daily News, linaripoti kuwa Bi Shosi ni mjane raia wa Kenya ambaye alikuwa ameolewa na raia wa Tanzania na aliishi mkoa wa Tanga.
Bwana Magufuli aliwaamrisha majaji kwa haraka kusikiliza kesi yake. Pia alimuamrisha jaji mkuu ambaye alikuwa kwenye mkutano huo kumpa mama huyo namba yake ya simu ili waweze kufuatilia naye kesi hiyo.
Pia magufuli alimuarisha mkuu wa polisi kuhakikisha kuwa Bi Shosi amepewa ulinzi wa kutosha.
Chapisha Maoni