Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuwa chini ya uongozi wake wasichana wa shule ambao hujifungua watoto hawataruhusiwa tena kurudi shuleni,
Rais magufuli alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kwenye mji wa Chalinze, takriban umbali wa kilomita 100 magharibi mwa mji mkuu Dar es Salaam.
Magufuli anasema kuwa mwanamume ambaye atapatikana na hatia ya kumpachika mimba mtoto wa shule, atafungwa jela miaka 30 na kutumia nguvu alizotumia kumpachika mimba msichana huyo, kufanya kilimo akiwa gerezani."Mashirika haya yasiyo ya serikali yanastahili kuenda kufungua shule kwa wazazi, lakini hayastahili kuilazimisha serikali kuwarejesha shuleni.
"Ninatoa elimu ya bure kwa wanafunzi ambao wameamua kusoma, na sasa nataka niwaelimishe wazazi," Rais Magufuli alisema.
Nchini Tanzania kuna takriban wasichana 8,000 ambao huacha shule kila mwaka kutokana na kuwa wajawazito, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch.
Chapisha Maoni