Watu waliondolewa kwa haraka katika eneo la Centro Andino mall, baada ya mlipuko kutokeaHaki miliki ya pichaNATALIO COSOY / BBC
Image captionWatu waliondolewa kwa haraka katika eneo la Centro Andino mall, baada ya mlipuko kutokea
Wanawake watatu wameuwawa, katika kile wakuu nchini Colombia wanasema kuwa, shambulio la kigaidi katika mji mkuu Bogota.
Mlipuko huo ulitokea katika soko moja la biashara la Zona Rosa, katika mji mkuu Bogota.
Watu wengine 11 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.
Meya wa Bogota, Enrique Penalosa, amesema kuwa mmoja wa wanawake aliyefariki anatoka Ufaransa.
Polisi wakipiga doria nje ya maduka hayoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi wakipiga doria nje ya maduka hayo
Wakuu wanaamini kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya choo cha wanawake, baada ya bomu dogo kulipuka.
Mlipuko huo ulitokea Jumamosi alasiri wakati wa shughuli nyingi, katika soko hilo la kibiashara, pale lilikuwa limejaa wateja, waliokuwa wakinunua bidhaa za siku kuu ya kina baba Duniani-- ambayo inasherehekewa leo siku ya Jumapili, Juni 18.
Rais Santos akiwa katika maeneo hayo ya maduka ya AndinoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionRais Santos akiwa katika maeneo hayo ya maduka ya Andino
Haijabainika ni nani au kundi lipi, lilitekeleza shambulizi hilo.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top