Miili kadhaa ya mabaharia waliokuwa wametoweka baada ya meli moja ya jeshi la majini la Marekani kugongana na meli moja ya mizigo katika pwani ya Japan, imepatikana.
Maiti hizo zilipatikana ndani ya meli hiyo katika kichumba cha kulala ambacho kiliharibika na kujaa maji.Mabaharia hao waliripotiwa kutoweka, baada ya meli USS Fitz-gerald kugongana na meli ya mizigo ya Ufilipino.
Ajali hiyo ilitokea kilomita 100 baharini eneo la Kusini magharibi mwa mji wa bandarini wa Yokosuka, nchini Japan saa nane unusu saa za Japan, jana Jumamosi.
Sehemu moja ya meli hiyo iliharibika kabisa, lakini ikafaulu kurejea katika kambi yake mjini Yokosuka, kwa msaada wa maboti ya jeshi la Marekani.Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikopta
Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.
Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.
Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.
- Meli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.
Chapisha Maoni