Wanajeshi saba wanamaji wa Marekani hawajulikani waliko baada ya meli yao USS Fitzgerald, kugongana na meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Ufilipino, katika pwani ya mashariki mwa Japan.

Walinzi wa pwani ya Japan wametuma maboti tano na ndege mbili katika eneo hilo kusaidia katika shughuli za uokozi.

Msemaji wa jeshi la maji la Marekani, amesema huenda maafisa hao wako sehemu za ndani za zilizofungwa ili kuzuia maji zaidi kuingia ndani ya manuari hiyo.Meli ya ACX Crystal ilionekana kugeuka kabla ya jali hiyo kabla ya kuelekea mjini Tokyo

Hakuna taarifa zozote zilizotolewa juu ya meli ya pili iliyokuwa na bendera ya Ufilipino ACX Crystal.

Kati ya waliojeruhiwa ni kamanda wa meli ya Marekani ambaye alipelekwa hospitalini kwa njia ya helikoptaUharibifu kwenye meli ya mizigo ya ACX

Meli hiyo ya kijeshi iligongwa na ile ya mizigo umbali wa kilomita 104 kusini magharibi mwa Yokosuka.

Picha zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye meli ya kijeshi baada ya ajali hiyo.Waliojeruhiwa wakiondolewa kutoka meli ya Japan

Haijulikani ni wapi meli hiyo ya urefu wa mita 154 ambayo ni ya kuharibu makombora ilikuwa ikielekea wakati huo.

Meli ya mizingo ya ACX Crystal yenye urefu wa mita 222 iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Ufilipo ilikuwa ikisafiri kati ya miji ya Japan ya Nagoya na Tokyo.YokosukaKWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top