Rais Dk John Magufuli amemwapisha Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo.
Kiapo hicho kinafuatia uteuzi alioufanya Rais Magufuli kwa Mwenyekiti huyo wa chama cha ACT – Wazalendo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mapema mwezi huu.
Mara baada ya kiapo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira alipanda gari lake la kazini na kuelekea Mkoani Kilimanjaro kuanza kazi rasmi. Mama Anna Mghwira anachukua nafasi ya Said Meck Sadiq ambaye aliomba kujiuzulu na kukubaliwa na Rais Dk John Magufuli.

Mkoa wa Kilimanjaro umepata kuongozwa na wakuu wa mkoa watatu katika kipindi cha miaka miwili, Leonidas Gama ambaye ni mbunge wa Songea Mjini, Said Meck Sadick na Anna Elisha Mghwira.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top