Jeshi nchini Iraq limethibitisha kwamba wanamgambo wa dola ya kiislam Islamic State wameulipua msikiti mkuu wa Al-Nuri ulioko mjini Mosul .
Msikiti huo unaaminika ndimo kiongozi wa wanamgambo wa IS Abu Bakr al-Baghdadi alitoa hotuba yake miaka mitatu iliyopita wakati alipokuwa akitangaza "ukhalifa" mpya.
Wakati hayo yakijiri, wanamgambo hao wa IS wao wanadai kwamba ndege za jeshi la Marekani ndiyo zilizo zilizousambaratisha msikiti huo.Mapema leo, Kamanda wa majeshi ya Iraq aliiambia BBC kwamba walikuwa mita kadhaa kutoka msikitini hapo, walipokuwa katika harakati zao za kusonga mbele kwenye mapambano lengo likiwa ni kuteka ngome kuu ya wanamgambo hao wa kiislam wa Is nchini Iraq.
Chapisha Maoni