BUNGE jana lilisimama kwa dakika moja kuendelea na shughuli zake kuishangilia timu ya Yanga iliyokuwa ikiingia kwenye ukumbi wa Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde.
Wakati wabunge wakiwa katikati ya kipindi cha maswali na majibu, wakihoji serikali kwa kuuliza maswali ya msingi na ya nyongeza, Kikosi cha Yanga kikaingia ukumbini na kukaa kwenye viti vya wageni saa 3.45 asubuhi ndipo wabunge mashabiki wa timu hiyo walianza kugonga meza kuishangilia. Kutokana na shamrashamra hizo, ilibidi Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga kuwaomba wabunge waache kugonga meza watulie ili waendelee na kipindi cha maswali na majibu.
Tofauti na ilivyokuwa ikiingia timu ya Mbao hakuna hata mbunge mmoja aliyeshtuka wala kushangilia, lakini wakati ikiingia Yanga, wabunge walivuruga utaratibu wa kuuliza serikali, wakaanza kugonga meza. Awali, akitoa matangazo ya wageni waliopo Bungeni, Mwenyekiti wa Bunge, Najma alisema miongoni mwa wageni waliopo ni timu ya Yanga ambao ni wageni wa Naibu Waziri Mavunde.
Wabunge tena waliibuka kwa shangwe kwa kupiga meza na kwa dakika mbili hivi waliendelea kushangilia hasa baada ya wachezaji waliovalia jezi za njano kusimama. Mwenyekiti Najma aliwataka mashabiki wa Simba bungeni wanyamaze kwani Yanga ni bingwa mara tatu na hata Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA) limeshaipongeza.
Akawataka mashabiki wa Yanga pekee ndio washangilie timu yao kutokana na kufanya vizuri katika ligi mwaka huu na kuwa bingwa kwa mara ya tatu. Yanga ipo kwenye ziara ya kuonyesha kombe kwa mashabiki wao ambapo ikitoka hapa inakwenda Arusha itakapocheza mechi ya kirafiki na AFC na Nyanza FC.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA TUPIGIE 0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top