Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha ametia saini mkataba mpya wa miaka mitano ya ziada katika klabu hiyo ya ligi ya England.
Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ivory Coast ameicheza timu hiyo na kufanikiwa kuifungia mabao 34 .
Zaha, mwenye umri wa miaka 24, ameuambia mtandao wa klabu hiyo: "Palace ipo moyoni mwangu na sidhani kwamba hadithi hii imemalizika."
Aliondoka Palace kujiunga na Manchester United mnamo 2013 kwa kitita cha pauni milioni 10 na baadaye kurudi katika klabu hiyo mnamo 2015 baada ya kuuzwa kwa mkopo London kusini.
Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Mwewe Steve Parish ameongeza: "Wilf amekuwa akiichezea klabu hii tangu akiwa miaka 8 na amekuwa katika kikosi cha kwanza tangu nilipowasili katika klabu hii. Yeye ndio bahati yetu na ni mtu ambaye hujitolea kikamilifu daima."
Chapisha Maoni