Manchester City wanatarajiwa kukamilisha unuzi wa £43m wa kiungo wa kati mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva kutoka kwa mabingwa wa ligi Ufaransa Monaco.
Silva, 22, atajiunga na City mnamo 1 Julai, na klabu hizo zinatarajiwa kutangaza rasmi uhamisho wake baadaye leo Ijumaa.
Mchezaji huyo ameichezea Monaco mechi 58 msimu huu, mbili dhidi ya City katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na kufunga mabao 11 na kusaidia ufungaji wa mabao 12.
Amechezea Ureno mechi 12 na kuwafungia bao moja.
Vijana hao wa Pep Guardiola walimaliza Ligi ya Premia wakiwa nafasi ya tatu, na kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.
Silva alisaidia Monaco kufika nusufainali ya michuano hiyo msimu huu ambapo walishindwa na Juventus.
Juventus watakutana na Real Madrid fainali Jumamosi tarehe 3 Juni.
Chapisha Maoni