Picha haihusiani na habari hapa chini
Wachimbaji wadogo wanne wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya Nyamalimbe yaliyopo wilayani Geita mkoani Geita.
Watu saba walifukiwa ambapo kati yao watatu wameokolewa na wamelazwa katika Kituo cha Afya Katoro.
Tukio hilo limetokea leo saa mbili asubuhi.
Mkuu wa Wilaya ya Geita ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya Herman Kapufi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Chapisha Maoni