Mchungaji wa kanisa la Divine mkazi wa Nyahanga mjini Kahama Beckam Gadson Joseph (24) amefariki dunia baada ya pikipiki aliyokuwa anaendesha yenye namba za usajili MC 446 AFP SANLG kugonga daraja na kupinduka katika eneo la Kiinza Majarubani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACM Muliro Jumanne Muliro mchungaji huyo wa kanisa la Divine alikuwa anatokea Kiinza kwenda Kahama mjini ndipo pikipiki aliyokuwa anaendesha kugonga daraja kisha kupinduka na kusababisha apoteze maisha.

Kamanda Muliro amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva huyo na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Kahama.

Na Kadama Malunde mkuu wawaandishi,
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top