MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga wanatarajia kukutana uso kwa uso na mabingwa wa Kenya Tusker katika michuano ya kuwania Kombe la Sportpesa itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Juni 5, mwaka huu.
Akizungumzia michuano hiyo jana Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa Sportpesa Abbas Tarimba alisema jumla ya timu nane za Tanzania na Kenya zinazodhaminiwa na kampuni hiyo ya bahati nasibu zitachuana kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Alisema kabla ya Yanga kukutana na Tusker saa 10:00 jioni, mchezo wa ufunguzi siku hiyo utachezwa saa nane mchana kati ya AFC Leopards dhidi ya Singida United. Aidha, Simba itacheza siku inayofuata dhidi ya Nakuru all Stars, wakati Gormahia ikitarajiwa kuchuana dhidi ya Jangombe boys ya Zanzibar.
Alisema timu mbili walizozialika na haziko kwenye udhamini wao ni Jangombe ya Zanzibar na Tusker ya Kenya na kuongeza kuwa michezo itakuwa ni hatua ya mtoano. Tarimba alisema mshindi wa kwanza atapata pesa dola za kimarekani 30,000 sawa na zaidi ya sh. Milioni 60 na mshindi wa pili dola za Marekani 10,000 sawa na zaidi ya sh. Milioni 12.
Alisema timu zitakazoingia nusu fainali zitaondoka na dola za kimarekani 5000 kila mmoja zaidi ya sh milioni 10 na washiriki wrote nane watapata kifuta jasho dola za kimarekani 2500 kila mmoja sawa na zaidi ya sh. Milioni 5.
Nusu fainali zitafanyika Juni 8, ambapo mechi ya kwanza itazikutanisha mshindi wa mechi kati ya Singida United dhidi ya AFC Leopard na mshindi kati ya Yanga na Tusker. Nusu fainali ya pili itazikutanisha mshindi kati ya Simba na Nakuru All Stars na Jang’ombe Boys dhidi ya Gor mahia.
Fainali itapigwa Juni 11. Alisema pesa zitakazopatikana kutokana na mauzo ya tiketi wakati wa ligi hiyo zitaelekea moja kwa moja katika maendeleo ya mpira wa miguu.
KAMA UNAMATANGAZO HABARI NYIMBO TUPIGIE 0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top