BAADHI ya wachezaji wa Azam FC waliomaliza mikataba yao wanadaiwa kugoma kusaini mikataba mipya ikidaiwa kuwepo kwa mabadiliko ya fedha za ada ya usajili.
Habari za uhakika kutoka Azam zinadai kuna kiongozi mmoja amekuwa akisisitiza kuwepo na kiwango maalum cha fedha watakazolipwa wachezaji kama ada ya kusaini mkataba tofauti na miaka ya nyuma ambapo mchezaji hulipwa baada ya kujadiliana na kufikia makubaliano na uongozi.
Aidha, pia inadaiwa kitendo cha kuondoka kwa mshambuliaji wao John Bocco anayedaiwa kusajiliwa na Simba kumewaumiza wengi kwani walikuwa wakihitaji huduma ya nahodha wao huyo. Wachezaji kadhaa wameshamaliza mikataba yao akiwemo Bocco, Aishi Manula na Salum Aboubakar. Chanzo cha habari ndani ya Azam kililiambia gazeti hili huenda wachezaji waliomaliza mikataba yao wakatimka kwenye timu nyingine watakaposhindwa kufikia muafaka na Azam.
“Chanzo cha mpasuko ni kiongozi mmoja (anamtaja) ambaye anataka kupunguza mishahara, kupunguza ada ya kusaini mkataba mpya na ndiye anayesababisha mpasuko kwa sababu anawakataa baadhi ya wachezaji kwa maslahi yake,” kilisema chanzo hicho.
Manula ambaye juzi alitwaa tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu msimu wa mwaka 2016/2017 bado hajasaini mkataba mpya na amekuwa akihusishwa kutakiwa na Singida United, Simba na Yanga. Chanzo hicho pia kilisema kuwa wachezaji walimzoea Bocco na kuondoka kwake kumewaumiza kwani hawalewi sababu za kutoongezewa mkataba na kwamba baadhi yao wanatamani kuachana na timu hiyo.
Alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, msemaji wa Azam, Jaffar Idd hakutaka kuzungumzia akidai hana taarifa. Kuhusu Bocco, Idd alisema wanamtakia kila la heri katika safari yake na kwamba tayari walishamalizana naye.
“Tutaendelea kumkumbuka daima, alikuwa na nidhamu kubwa kwa kipindi ambacho ametumikia hapa,” alisema. Alisema walikuwa kwenye kikao kizito jana na huenda kuna wachezaji wengine wakapewa barua za kuachana na klabu hiyo.
KWA HABARI ZA BIASHARA NYIMBO''0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top