Rashamba, Debola, mwanamke mzee wa kabila la Ogiek
Image captionRashamba Debola, wa kabila la Ogiek anasema "nilizaliwa katika msitu wa Mau, nikaolewa hapa kitamaduni, nikazaa hapa, na nikamzika mume wangu katika msitu huu."
Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu mjini Arusha Tanzania imetoa uamuzi muhimu kuwaruhusu watu wa kabila la Ogiek nchini Kenya - mojawapo ya makabila madogo sana ya Kiasili nchini humo kurudi katika ardhi waliokuwa wanaishi msitu wa Mau.
Jamii ya kabila hilo la jadi la Ogiek ni ndogo na inajumuisha wawindaji wanaoishi katika msitu wa Mau katika mkoa wa bonde la ufa Kenya.
Jamii hiyo iliwasilisha kesi dhidi ya serikali ya Kenya katika jitihada za kuruhusiwa kuendelea kumiliki ardhi yao na rasilmali zao.
Mahakama hiyo ya haki za binaadamu sasa imeamua kuwa serikali ya Kenya haikupaswa kuitimua jamii hiyo ya Ogiek kutoka msitu wa Mau kwasababu ardhi hiyo ni yao ya jadi.
Jamii ya kabila la Ogiek nje ya mahakama ya haki za binaadamu Arusha
Image captionJamii ya kabila la Ogiek nje ya mahakama ya haki za binaadamu Arusha
Mahakama imepuuzia tuhuma za serikali kwamba imeamua kuitumia jamii hiyo ili kuuhifadhi msitu, badala yake mahakama imesema maafisa nchini kenya wameshindwa kuidhihirishia mahakama kwamba jamii hiyo ya watu wa Ogiek wanaleta madhara yoyote kwa msitu huo.
Aidha imeongeza kuwa serikali ya Kenya imekiuka haki za watu wa jamii hiyo ikiwemo haki za kitamaduni, haki ya kutambuliwa katika suala la rasilmali za kitaifa, na pia wamenyimwa haki ya kumiliki mali.
Mnamo Julai 2008, serikali ya Kenya iliwatimua kwa nguvu watu wanaoishi katika msitu wa Mau ikiwemo jamii hiyo ya Ogiek - ikidai kwamba wanaishi katika sehemu hiyo kinyume cha sheria,.
Hatua hiyo ilikuwa ndio kilele cha mvutano wa muda mrefu uliokuwa unashuhudiwa kati ya jamii ya Ogiek na serikali ya Kenya.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top