MWANZA,
Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo.
Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.
Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .
Chapisha Maoni