Francesco TottiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTotti aliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo aliyoichezea kwa miaka 25
Francesco Totti alitokwa na machozi alipokuwa anaaga baada ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya AS Roma.

Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 40 amechezea klabu hiyo kwa miaka 25.
Katika kipindi hicho, amefunga mabao 307 katika mechi 786 alizocheza.
Aliingia uwanjani mara ya mwisho dakika ya 54 mechi yao dhidi ya Genoa.
Roma walishinda 3-2 kupitia bao la dakika ya mwisho la Diego Perotti ambalo liliwahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Baada ya mechi, Totti alisoma barua kwa mashabiki, na kusema: "Naogopa. Sijui siku za usoni zitakuwaje."
Francesco TottiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFrancesco Totti alitokwa na machozi baada ya mechi alipopewa ubao wa nambari 10 kwenye fremu. Mashabiki waliinua mabango yenye nambari hiyo ya jezi yake.
"Tafakari, kwamba wewe ni mtoto na umo katikati ya ndoto nzuri...na mamako anakuamsha uende shuleni.
"Unajaribu kurejea kwenye ndoto yako...unajaribu sana lakini huwezi.
"Wakati huu si kwamba ni ndoto, ni uhalisia. Na siwezi kurejea tena."
Nahodha Totti pia alipewa nambari 10 iliyowekwa kwenye fremu, nambari ya jezi yake.
Mkewe na watoto pia walikuwa uwanjani.
Anatarajiwa kuwa mkurugenzi katika klabu ya Roma lakini kumekuwepo na taarifa kwamba huenda akaelekea kwingine.
Francesco TottiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionFrancesco Totti akirushwa juu na wachezaji wenzake
Robocap bannerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRobocap, lilisema bango moja, kwa heshima ya mchezaji huyo aliyekuwa nahodha wa Roma kwa miaka 18
Roma bannerHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAmore Infinito - upendo wa milele - lilisema bango jingine
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top