CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewaomba Watanzania wote kumuunga mkono Rais John Magufuli kutetea maslahi ya nchi ikiwa ni pamoja na kuunga mkono hatua ya kudhibiti rasilimali za madini ya dhahabu nchini.
Katibu wa Sekretarieti, Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole (pichani) alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia hatua ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo kwa madai ya kushindwa kusimamia sekta ya madini nchini. Polepole aliwaomba Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli kwani ni moja ya jambo litakalozidi kumuweka imara na madhubuti zaidi kikazi.
Rais Magufuli alimtimua waziri baada ya kupokea ripoti ya Kamati Maalumu iliyochunguza kilichomo katika kontena 277 zilizokuwa na makinikia ambapo ilibainika kuwepo upotevu wa dhahabu ya sh trilioni 1.4. Katika ripoti hiyo ilibainika kuwepo kwa takwimu za uongo jambo ambalo liliikosesha serikali mabilioni ya fedha kwa miaka 19 tangu biashara hiyo ya kusafirisha nje ya nchi makinikia maarufu kwa mchanga wa dhahabu ianze.
“Kazi kubwa ya CCM ni kuwa bora leo kuliko jana, tumedhulumiwa sana mali tulizorithi, ipo haja na kizazi cha sasa kirithishe kwa kizazi kijacho,” alisema Polepole. Alisema haki itabaki kuwa haki na awamu ya tano ya uongozi inajinasibu ili rasilimali zitumike kwa upana na kila Mtanzania. Alisema haiingii akilini mchanganuo wa kifedha wa thamani ya mchanga huo umekuwa hivyo wakati awali ikitolewa viwango tofauti visivyostahili jambo linalooonesha wametumia ujinga wa Watanzania kuchuma mali.
“Hawa ni maharamia wa kiuchumi, walijaribu kuhonga sh bilioni 300 kabla ya ripoti kutolewa lakini Rais Magufuli aliwakatalia na kuwataka wasubiri uchunguzi ukamilike,” alisema Polepole. Alisema CCM mpya ni chachu ya maendeleo hivyo ni vyema kusimama pande zote kumpa moyo kiongozi huo kwa kuwa jambo hilo ni la kipekee.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA ,NYMBO WASILIANA NASI 0623372368
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top