MKAZI wa Kijiji cha Nyiboko Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara, Mgonchori Mwita Bonchori (28) maarufu Kisine, amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake, Nchato Nyansemo kwa kumkata shingo mara tatu kwa kutumia panga, akidai kutukanwa na kukataliwa na mpenzi wake huyo.
Jaji Rose Ebrahim alisoma hukumu hiyo jana katika kikao cha Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, kilichofanyika katika Mahakama ya Wilaya Tarime. Alisema katika kesi hiyo ya mauaji namba 84 ya 2013, anakubaliana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, Mwanasheria wa Serikali, Venance Mayenga.
Awali, mwanasheria huyo alidai kuwa mtuhumiwa huyo Oktoba 20, 2011 alikwenda kwenye baa akiwa na panga kwa nia ovu ya kutenda kosa kwa mpenzi wake, aliyefahamika kwa jina Nchota.
Alimkuta mpenzi wake huyo mahali hapo na kuanza kumshambulia kwa kumkata kwa panga mara tatu shingoni na kusababishia kifo chake kutokana na kutokwa damu nyingi. Mwanasheria huyo alidai kuwa, Mgonchori alipokamatwa alikiri kufanya mauaji hayo.
Alikiri pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nchota na kwamba mpenzi wake huyo alimkasirisha kwa kumtukana kuwa ni mpumbavu na kumkataa kimapenzi, hali iliyomfanya akasirike na kumkata kwa panga shingoni hadi kumsababisha umauti.
Wakili wa mtuhumiwa, Baraka Makowe alidai mahakamani hapo kuwa mteja wake, Mgonchori, wakati anatenda kosa hilo alikuwa amelewa na aliiomba mahakama hiyo imshitaki kwa makosa ya kuua bila kukusudia.
Hata hivyo, Jaji Ebrahim aliungana na upande wa mashitaka, akisema bila ya shaka yoyote mtuhumiwa alifanya mauaji kwa kukusudia chini ya Kifungu cha 196 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwani mtuhumiwa alikiri kumkata panga mara tatu marehemu aliyedai kuwa ni mpenzi wake.
Alisema; “Kitendo cha mtuhumiwa Mgonchori cha kwenda baa akiwa na panga alikuwa na nia ovu na alidhamiria kutenda kosa hilo, nguvu zilizotumika zilikuwa kubwa, silaha aliyotumia katika tukio hilo yaani panga, mbali na mtuhumiwa kudai kuwa alitenda kosa hilo akiwa amelewa pombe alikunywa yeye mwenyewe bila kunyweshwa na mtu yeyote.
“Hakuna taarifa zilizoonesha kuwa wakati wa kutenda kosa, alikuwa ameleweshwa, hali inayoonesha wakati anatenda mauaji hayo alikuwa na akili timamu.” Katika hukumu yake, Jaji alisema: “Kutokana na kitendo cha ukatili uliofanya …ninakuhukumu adhabu ya kunyon
Chapisha Maoni