Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia akipokea msaada wa
Madawati, kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Nyaligogo
Masumbuko Lushona kushoto, ili kupungufa upungufu wa madawati katika
shule ya Msingi Nyaligongo wilayani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Wananchi
wa kijiji cha Nyaligongo Kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wametoa
msaada wa madawati 100 katika shule ya Msingi Nyaligongo, ili kumaliza
tatizo la upungufu wa madawati shuleni hapo.
Msaada
huo wa madawati umetolewa jana shuleni hapo, na kupokelewa na Mkuu wa
Wilaya ya Shnyanga Jasinta Mboneko, ili kuboresha mazingira mazuri ya
wanafunzi kusoma na kutimiza ndoto zao.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho cha Nyaligongo Masumbuko Lushona, amesema fedha za
utengenezaji huo wa madawati zimechangwa na wananchi kwa lengo la
kuondoa adha ya wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini, na sasa wapo
kwenye ukamilishaji wa madawati mengine 100.
“Wananchi
wa kijiji hiki cha Nyaligongo tunaungana na Serikali kuboresha
miundombinu ya elimu, ili watoto wetu wasome katika mazingira mazuri na
kupata ufaulu mzuri na kutimiza ndoto zao, na kuja kuwa msaada kwetu
hapo baadae,”amesema Lushona.
Nao
baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo akiwemo Zephania Daudi anayesoma
darasa la nne , amesema wanafunzi wanapokuwa wakisoma huku wamekaa
chini, ufanisi wa kusoma hua ni mdogo huku wakikabiliwa na miandiko
mibaya, lakini wakikaa juu ya madawati usomaji wake huwa ni tofauti
pamoja na kuwa ni miandiko mizuri.
Naye
Mwanafunzi Elizabeth Maduhu, amesema uwepo wa madawati ya kutosha
shuleni, hata ufaulu wa wanafunzi utaongezeka pamoja na kupunguza utoro,
sababu ya kuwapo na mazingira mazuri ya kujisomea na kutimiza ndoto
zetu.
Aidha
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Emmanuel Raymond, amesema shule hiyo ina
jumla ya wanafunzi 1,300 na inakabiliwa na upungufu wa madawati 250.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewapongeza
wananchi hao kwa kuchangia madawati hayo, huku akiwataka wanafunzi
wasichole chole madawati hayo pamoja na kupanda juu ili yasivunjike,
bali yadumu kwa muda mrefu na kusoma katika mazingira mazuri.
Katika
hatua nyingine Mboneko amewaonya wazazi na walezi, kuacha tabia ya
kuwarubuni wanafunzi wa kike wafanye vibaya kwenye mitihani yao, ili
wapate mwanya wa kuwaozesha ndoa za utotoni kwa tamaa ya kupata mali,
bali wawaache watimize ndoto zao na kuja kuwasaidia hapo baadae.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kulia), akikabidhiwa madawati
100 na uongozi wa Serikali ya kijiji cha Nyaligongo kwa ajili ya
kupunguza upungufu wa madawati katika shule ya msingi Nyaligongo,
kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha Nyaligongo Masumbuko Lushona.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanafunzi wa
shule ya Msingi Nyaligongo wilayani Shinyanga na kuwataka wasiharibu
madawati hayo, bali wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akiendelea kuwapa nasaha wanafunzi wa shule ya Msingi Nyaligongo juu ya kupenda elimu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Nyaligongo Emmanuel Ryamond, akizungumza mara baada ya kupata msaada huo wa madawati.
Mwanafunzi
wa shule ya Msingi Nyaligongo Elizabeth Maduhu, akielezea faida ya
shule kuwa na madawati ya kutosha na kushukuru kupatiwa madawati hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na
baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Nyaligongo mara baada ya
kumalizika kwa zoezi la upokeaji wa madawati 100.
Chapisha Maoni