Muhubiri mwenye utata Gilbert Deya amerudishwa nchini Kenya ambapo anakabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa watu.
Deya aliwasili nchini Kenya siku ya Ijumaa akiabiri ndege ya KQ.
Hii ni baada ya rufaa yake dhidi ya hatua ya kumrudisha nchini Kenya kukataliwa na mahakama ya Uingereza.
Muhubiri huyo anamiliki kanisa moja eneo la Peckham kusini mashariki mwa mji wa London.Amekuwa katika orodha ya watu wanaosakwa kwa ulagunzi wa binaadamu tangu 2004.
Mwaka 2014 , mahakama moja ya London ilimwachilia muhubiri huyo kwa mashtaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono.
Amekana mashtaka yote.
Mkewe bi Mary Deya alifungwa jela mwaka 2014 baada ya kupatikana katika kitengo cha watoto katika hospitali ya Kenyatta 2005.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 3 na jaji wa mahakama kuu Msagha Mbogholi.
Kaimu Grace Nzioka alikuwa amemfunga Mary 2011 kwa wizi wa mtoto mmoja na kutoa habari za uwongo lakini alikata rufaa dhidi ya shtaka hilo.
Chapisha Maoni