Kombora la Korea Kaskazini lilikaribia ndege ya UfaransaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKombora la Korea Kaskazini lilikaribia ndege ya Ufaransa
Ndege moja ya Ufaransa iliokuwa na abiria 330 ilikuwa kilomita 100 pekee na kombora la masafa marefu lililorushwa na Korea Kaskazini maafia wanasema.
Ndege hiyo ilipita katika eneo ambalo kombora hilo lilinguka dakika 10 baadaye .
Kampuni ya Airfrance inasema kuwa ndege yake haikuwa hatarini lakini imejiweke marufuku ya kusafiri katika anga ya Korea Kaskazini kama tahadhari.
Pentagon inasema kuwa kombora hilo lilipaa katika anga yenye shughuli nyingi.
Maafisa wa Marekani nara kwa mara wamekuwa wakionya kuhusu hatari zinazoletwa na makombora dhidi ya ndege za abiria katika eneo hilo.
Kombora la masafa marefu ICBM
Image captionKombora la masafa marefu ICBM
Njia iliotumiwa na ndege hiyo aina ya Boeing 777 inaonyesha kuwa ilikuwa magharibi, mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa la Japan , wakati bora hilo la Korea Kaskazini lilikuwa hewani.
Japan na Marekani inakadiria kwamba kombora hilo lilianguaka kati ya kilomita 100na 150 karibu na ndege hiyo.
"Kombora hilo liliruka katika anga na kuanguka nchini Japan, eneo ambalo hutumika na vyombo vya kibiashara na vile vya uvuvi , msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top