Ikiwa ni siku chache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini Kenya, Muungano wa Upinzani (NASA) umeishutumu serikali kuwa imevamia moja ya vituo vyake vya kuhesabia kura kilichopo eneo la Westlands jijini Nairobi.


Msemaji wa NASA ameeleza kuwa wanaume waliokuwa wamefunika nyuso zao walivamia ofisi hiyo wakafanya uharibifu na kubeba kompyuta, simu za mkononi na vitabu.


Kwa upande wake, serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa hakuna uvamizi uliofanyika, . Mgombea wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa atakubali tu kushindwa ikiwa uchaguzi utakuwa wa haki.

Hivi karibuni, Rais wa Uhuru Kenyatta alikaririwa akisema ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo wa siku ya Jumanne licha ya kila mmoja kusisitiza kuwa ataibuka mshindi.

Uchaguzi wa Kenya mara nyingi umekua ukikumbwa na ghasia. Zaidi ya watu 1000 waliuawa wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top