WAZIRI anayeshughulikia sekta ya usafirishaji nchini Uganda, Bagiire Aggrey Henry ameusifu Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) kwa jinsi unavyorahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo kutoka eneo la Kivukoni Manispaa ya Ilala hadi kituo cha Morocco, Kinondoni, waziri huyo aliyeongozana na ujumbe wa Serikali yake kuja nchini, alisema Mradi wa BRT umekuwa na mafanikio makubwa na umesaidia kuondoa msongamano mkubwa wa magari.
“Tumefurahi kuuona mfumo wenu wa Mabasi Yaendayo Haraka unavyofanya kazi, nasi tukirudi Uganda tutakwenda kutekeleza kile tulichokiona, maana tuna mpango wa kuanzisha mfumo kama huu katika jiji la Kampala,” alisema Bagiire.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho aliyemwakilisha Waziri, Profesa Makame Mbarawa alisema Mradi wa BRT umekuwa kivutio kikubwa kwa wageni, ndiyo maana viongozi hao kutoka Uganda waliomba kuutembelea.
Chapisha Maoni