WhatsAppHaki miliki ya pichaWHATSAPP
Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa Kenya imewatahadharisha wasimamizi wa makundi ya mawasiliano katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwamba watachukuliwa hatua makundi yao yakitumiwa kueneza chuki.
Tume hiyo imesema kwamba itakabiliana vilivyo na watu watakaotoa matamshi ya chuki na kikabila nchini humo, wakati huu wa kampeini za uchaguzi mkuu.
Uchaguzi mkuu nchini Kenya utafanyika mnamo tarehe 8 mwezi Agosti.
"Enyi wasimamizi wa makundi ya WhatsApp ambao makundi yenu yanatumiwa kusambaza ujumbe wa chuki, hebu tuwe makini," amesema mwenyekiti wa tume hiyo Francis Kaparo, ambaye zamani alikuwa spika wa bunge la Kenya.
Amesema tume hiyo imeyatambua makundi zaidi ya 21 ya WhatsApp ambayo yanatumiwa kueneza chuki.Bw Kaparo pia amewaonya wanasiasa ambao watatoa matamshi ya uchochezi, matusi, taarifa za uongo, yanayodhalilisha mtu au watu kingono au ya kukudunisha kikabila.
Bw Kaparo amesema "watakiona cha mtema kuni".
Aidha watumiaji wa simu za rununu pia wameonywa dhidi ya kusambaza ujumbe ambao unaweza kusababisha taharuki au vita vya kikabila.
WhatsAppHaki miliki ya pichaEPA
Polisi wameshauriwa kuwakamata watu wanaokiuka tahadhari hiyo iliyotolewa huku kampuni za rununu na mitandao ya kijamii zikiombwa kuondoa ujumbe ambao wanaona unaweza kuingiza taifa katika lindi la vita na umwagikaji wa damu.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya Joseph Boinnet mapema leo Jumatatu, amesema kuwa kikosi chake "kitatumia nguvu zaidi" dhidi ya watakaosababisha vurugu.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/08, zaidi ya watu 1,133 waliuawa na zaidi ya watu nusu milioni wakaachwa bila makao baada ya ghasia kuzuka.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top