Picha hii ya Mtandao inawaonesha watoto wa Kimasai wakiwa katika harakati za kutafuta maji kijijini kwao.
WANAFUNZI 12 wa jamii ya wafugaji wa Kimasai kati yao saba wa kike kutoka Shule ya Sekondari Parakuyo, wilayani Kilosa, Morogoro wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kuozeshwa, mimba za utotoni na utoro.
Hayo yamethibitishwa hivi karibuni na Mkuu wa shule hiyo, Peter Mruma alisema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe, katika Kata ya Parakuyo, Kilosa.
Alisema, kati ya wanafunzi hao, saba ni wa kike na watano wa kiume na walishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuozeshwa, mimba za utotoni na utoro kwa wavulana.
Shule hiyo ya bweni ilianzishwa mwaka 2007 na jamii ya wafugaji wa mkoa wa Morogoro na ilianza na wanafunzi 80 wakiwemo wasichana 40 na wavulana 40. Hata hivyo, alisema, katika waka huu wa masomo, shule ina jumla ya wanafunzi 222 kati yao wavulana 105 na wasichana 117 ikiwa na jumla ya walimu 12.
Dk Kebwe, akiwahutubia wakazi wa Parakuyo ambao asilimia kubwa ni wafugaji wa jamii ya Kimasai alisema “Naagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilosa, hakikisheni wahusika wote bila kujali umri ama ni kiongozi wa kimila, wapatikane na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria”.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top