Wapinaji wa Taliban wamewaua wanajeshi 26 wa Afghanistan wakati wa shambulizi kwenye kambi yao karibu na mji wa Kandahar
Msemaji wa wizara wa ulinzi alisema kuwa mapigano makubwa yameendelea eneo na vikosi zaidi vimetumwa.
Wanajeshi 13 walijeruhiwa wakati wa mapigano hayo ya usiku kucha.
Taliban wanasema kuwa wamedhibiti kambi hiyo iliyo wilaya ya Khakrez.
Hii ni moja ya misururu ya jeshi kushindwa na wanamgambo miezi ya hivi karibuni.
Taarifa za kijasusi nchini Afghanistan ziliiambia BBC mapema kuwa zaidi ya wanajeshi 40 waliuwawa.Wakaazi wa eneo hilo walisema kuwa mamia ya wanamgambo walishambulia kambi kutoka pande zote wakati wa shambulizi hilo lililodumu saa kadhaa.
Baada ya kuteka sehemu nyingi za mkoa wa Helmand miezi ya hivi karibuni, Taliban wamefanya mashambulizi kadhaa mjini Kandahar na sehemu zingeni za nchi.
Mwezi Mei wanamgambo hao waliteka kambi wa kijeshi eneo la Shah Wali Kot huko Kandahar.
Mwezi Aprili wanajeshi 170 waliuwawa wakati wa shambulizi la Taliban kwenye kambi ya jeshi eneo la Mazar-e Sharif
Chapisha Maoni