Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefunguka na kuahidi kuwa bado ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo.


Ameyasema hayo jana alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, ambapo alisema kuwa maendeleo ya nchi hayana vyama ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.


“Maendeleo hayana chama ndiyo maana unaona nimeweza kuteuwa baadhi ya viongozi kutoka tena kwenye chama kidogo, na nitaendelea kuchomoa watu wenye akili akili kutoka kwenye vyama mbalimbali nitawaacha vilaza huko huko,”alisema Rais Dkt. Magufuli


Hata hivyo, kwa upande wake, Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni mwanachama wa ACT- Wazalendo ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wananchi na kutambulishwa alifunguka na kusema kuwa, Rais Magufuli amevunja mwiko wa Serikali kuwa ikiongozwa na watu kutoka chama kimoja baada ya kumteua yeye kuwa Katibu Mkuu wa Maji pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Elisha Mghwira ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top