Mtoto aliyekanyagwa na gari enzi za uhai wake 


Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja amefariki dunia papo hapo leo usiku Jumatatu Julai 24,2017 baada ya kukanyagwa na gari wakati dereva akirudisha gari lake nyuma bila kuchukua tahadhari.



Tukio hilo limetokea usiku huu nyumbani kwao na mtoto huyo katika mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.

Kwa Mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo na kata hiyo,David Nkulila amesema mtoto huyo amekanyagwa na gari hilo linalodaiwa kuwa ni la serikali nyumbani kwao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook,Nkulila ameandika maneno yafuatayo:


HABARI ZA MAJONZI,,,,,,,, HUZUNI, Very BAD NEWS!!!!!
Nimepokea taarifa za kuhuzunisha saana usiku huu, nikiwa nyumbani, vijana wamenikuta usiku huu na kunijulisha kuwa kuna mtoto mdogo kakanyagwa na gari wakati Dereva akurudi nyuma,,,, Eeee Mungu!! akiwa hajui kuna mtoto nyuma ya gari,,,,,, alimkanyaga mtoto huyo (nimeambiwa umri ni kama mwaka 1na miezihivi)sehemu za kichwani,, KAFARIKI hapohapo. Nmeumia saana,,,,,, sijui niseme nini Mungu,,,,,!!! zaidi wana mtaa wa Mabambasi tutajulishana, msiba upo kwa Marehemu Kulwa Mzee,,,,, barabara ya phantom. Mungu amrhemu malaika wake APUMZIKE kwa amani.
Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top