South Korean solders at a border villageHaki miliki ya pichaCHUNG SUNG-JUN
Image captionKorea Kusini yataka mazungumzo na Korea Kaskazini
Korea Kusini imependekeza kufanyika mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya majuma kadhaa ya msukosuko, kufuatia hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya majaribio ya makombora.
Ikiwa mazungumzo hayo yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu tangu mwaka 2015.Maafisa wa vyeo vya juu walisema kuwa mazungumzo hayo yatalenga kisitisha vitendo vyote vyote ambavyo huchangia kuwepo misikusuko ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali kati ya Kusini Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.
North Korean TV releases photos of Tuesday's missile launchHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKorea Kaskanzini imekuwa ikifanyia makomboa majaribio
Akitoa hotuba hivi majuzi mjini Berlin, alisema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili kufanyika na kutaka muafaka kuafikiwa.
Lakini hatua za Korea Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwemo la hivi majuzi la masafa marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.Naibu waziri wa ulinzi nchini Korea Kusini Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.

KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE   SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top