Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk Vicent Mashinji, Mbunge wa Viti Maalum wa Chama hicho mkoa wa Ruvuma, Zubeda Sakuro pamoja na wanachama wengine kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na maandamano kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuwa, Gemini Mushi amesema Dk Mashinji na Mbunge huyo waliongoza maandamano hayo huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria.
Aliwataja wanachama wengine wanaoshikiliwa kuwa ni Sanuda Manawa, Katibu wa Ulinzi wa Taifa wa Chadema aliyetajwa kwa jina moja la Zuber, Fecil David, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini ambaye ni Charles Leonard.
Wengine ni Charles Makunguru ambaye ni Katibu Mwenezi Kanda ya Kusin, Filbert Ngatunga ambaye ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kusini na bado kazi ya ukamataji inaendelea kwa waandamanaji wengine ili hatua za kisheria zichkuliwe dhidi yao Kamanda Mushy amesema Mbunge huyo wa Viti Maalum aliomba kufanya kikao cha ndani na baadaye akaibuka na maandamano na viongozi wa chama hicho kutoka sehemu mbalimbali za nchI jambo ambalo lilizuiliwa.
Kwa mujibu wa Kamanda Mushy, maandamano hayo yalihusisha misafara ya watu na pikipiki zaidi ya 15 ambazo zilibeba abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki ambao walileta fujo ktk maeneo mbalimbali ya barabara za wilaya ya Nyasa.
Aidha Kamanda Mushy amewashauri wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kufanya shughuli zao za maendeleo kwani kipindi hiki siyo cha kufanya mikutano au mikusanyiko ya kisiasa badala yake watumie wasaa huo katika kufanya shughuli zao za maendeleo zitakazowaingizia kipato chao wenyewe na taifa kwa jumla.
Chapisha Maoni