Israil imeweka kamera pahala wa kuingia katika uwa wa msikiti wa al-Aqsa katika mji mkongwe wa Jeruslem.
Hayo yanatokea wakati wa mvutano mkubwa kuhusu hatua za usalama kwenye eneo hilo, ambalo waislamu wanali-ita Haram al-Sharif na wayahudi wanaita Temple Mount.
Waumini wa Palestina wamepinga vikali Israil kuweka mitambo ya kun'gamua kama mtu amebeba kitu cha chuma, baada ya askari polisi wawili wa Israil kuuwawa.Wapalestina watatu waliuawa wakati wa ghasia na vikosi vya Israel siku ya Ijumaa, wakati maelfu waliandamana mashariki mwa Jerusalem na eneo la linalomilikiwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.
Baadaye raia watatu wa Israel wakauawa kwa kuchomwa visu katika makao ya walowezi wa kiyahudi karibu na Ramallah na mshambuliaji mpalestina ambaye aliingia nyumbani kwao.
Chapisha Maoni