Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.



Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri.


Mawakili watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, waliiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Lissu ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema, “kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.”



Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 ambapo hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.

==>Hii ndpo hati ya shitaka lake


Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Chapisha Maoni

 
Top