Mchezaji namba tano kwa ubora wa mchezo tenesi Roger Federer ameweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji la michuano ya Wimbledon, kwa mara nane.
Federer ametwaa taji hilo la Grand Slam baada ya kumshinda mpinzani wake Marin Cilic, kwa jumla ya seti tatu.
Katika seti ya kwanza bingwa huyu wa kihistoria alishinda kwa 6-3, kisha akashinda kwa 6-1 na kumaliza kwa 6-4, katika mchezo ulichezwa kwa muda wa saa moja na na dakika 41.
Hili ni taji la 19 la Grand Slam, kwa mchezaji huyu raia wa Switzerland, na kuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi ya England.
KWAMATANGAZO YA BIASHARA KWAYA NYIMBO AINA ZOTE HABARI YEYOTE TUPIGIE SASA KWA NUMBE,WHATSAPP FB //+255 623372368=+255768163863
Chapisha Maoni