Mshindi wa taji la Wimbedon Roger Federer amepanda kwenye viwango vya ubora wa mchezo huo kutoka nafasi ya tano mpaka nafasi ya tatu
Mwingereza Andy Murray anaendelea kuwa kinara katika nafasi ya kwanza, Rafael Nadali akifuatia katika nafasi ya pili, Novak Djokovic ni namba nne kwa ubora, huku Stan Wawrinka akiwa katika nafasi ya tano.
Kwa upande wa wanawake Karolina Pliskova ndie kinara akifuatiwa na Simona Halep
Mjerumani Angelique Kerber yuko katika nafasi ya tatu na Johanna Konta akishika nafasi ya nne na Garbine Muguruza anakamilisha tano bora .
Chapisha Maoni